1 Samuel 4:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena ilitokea kwamba, mkwewe Eli, yaani mke wa Finehasi, wakati huo alikuwa mjamzito, na muda wake wa kujifungua ulikuwa umekaribia. Aliposikia kwamba sanduku la agano la Mungu limetekwa na kwamba baba mkwe wake, hata na mumewe wamefariki, mara moja alipata utungu, na kujifungua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkwewe, mke wa Finehasi, alikuwa mjamzito na alikaribia wakati wa kujifungua. Aliposikia habari kwamba Sanduku la Mungu limetekwa na ya kuwa baba mkwe wake na mumewe wamekufa, akapata uchungu naye akajifungua lakini akazidiwa na uchungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena ilitokea kwamba, mkwewe Eli, yaani mke wa Finehasi, wakati huo alikuwa mjamzito, na muda wake wa kujifungua ulikuwa umekaribia. Aliposikia kwamba sanduku la agano la Mungu limetekwa na kwamba baba mkwe wake, hata na mumewe wamefariki, mara moja alipata utungu, na kujifungua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkwewe, mke wa Finehasi, alikuwa mja mzito na karibu wakati wa kujifungua. Aliposikia habari kwamba Sanduku la Mungu limetekwa na yakuwa baba mkwe wake na mumewe wamekufa, akapata utungu naye akajifungua lakini akazidiwa na utungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkwewe, mke wa Finehasi, alikuwa mjamzito na karibu wakati wa kujifungua. Aliposikia habari kwamba Sanduku la Mungu limetekwa na ya kuwa baba mkwe wake na mumewe wamekufa, akapata utungu naye akajifungua lakini akazidiwa na utungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja mzito, karibu ajifungue; basi, aliposikia kuhusu kutwaliwa kwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha na kujifungua; maana uchungu wake ulimfikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena ilitokea kwamba, mkwewe Eli, yaani mke wa Finehasi, wakati huo alikuwa mjamzito, na muda wake wa kujifungua ulikuwa umekaribia. Aliposikia kwamba sanduku la agano la Mungu limetekwa na kwamba baba mkwe wake, hata na mumewe wamefariki, mara moja alipata utungu, na kujifungua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkwewe, mkewe Pinehasi, alikuwa mwenye mimba iliyokomaa; alipopashwa hizo habari za kutekwa kwake Sanduku la Mungu nazo za kufa kwake mkwewe na mumewe, akaanguka magotini, akazaa, kwani alishikwa na uchungu wake wa kuzaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena ilitokea kwamba, mukwe wa Eli, ni kusema muke wa Finehasi, kwa wakati ule alikuwa na mimba, na muda wake wa kuzaa ulikuwa umekaribia. Aliposikia kwamba Sanduku la Agano la Mungu limetekwa na kwamba baba mukwe wake, hata na mume wake wamekufa, mara moja akapata maumivu ya kuzaa. Kwa hiyo akachutama na kuzaa.