1 Samuel 4:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafilisti waliwashambulia Waisraeli, na baada ya mapigano makali, Waisraeli walishindwa. Waisraeli 4,000 waliuawa kwenye uwanja wa mapambano.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wafilisti wakapanga safu za majeshi yao kupambana na Israeli, wakati vita vilipoenea, Israeli wakashindwa na Wafilisti, ambao waliwaua askari wa Israeli wapatao elfu nne kwenye uwanja wa vita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Israeli wakapigwa mbele ya Wafilisti; wakauawa watu wa jeshi lao lililokuwa uwandani wapata watu elfu nne.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafilisti waliwashambulia Waisraeli, na baada ya mapigano makali, Waisraeli walishindwa. Waisraeli 4,000 waliuawa kwenye uwanja wa mapambano.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wafilisti wakapanga safu za majeshi yao kupambana na Israeli, wakati vita vilipoenea, Israeli wakashindwa na Wafilisti, ambao waliwaua askari wa Israeli wapatao 4,000 kwenye uwanja wa vita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wafilisti wakapanga safu za majeshi yao kupambana na Israeli, wakati vita vilipoenea, Israeli wakashindwa na Wafilisti, ambao waliwaua askari wa Israeli wapatao 4,000 kwenye uwanja wa vita.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Waisraeli wakapigwa na Wafilisti; waliowaua karibu elfu nne katika uwanja wa vita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafilisti waliwashambulia Waisraeli, na baada ya mapigano makali, Waisraeli walishindwa. Waisraeli 4,000 waliuawa kwenye uwanja wa mapambano.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Wafilisti wakajipanga kuwaelekea Waisiraeli; mapigano yalipoenea pakubwa, Waisiraeli wakapigwa na Wafilisti, hao wakaua watu kama 4000 papo hapo porini, walipojipanga kupigana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Israeli wakapigwa mbele ya Wafilisti; wakauawa watu wa jeshi lao lililokuwa uwandani wapata watu elfu nne.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafilistini waliwashambulia Waisraeli, na nyuma ya mapigano makali, Waisraeli walishindwa. Waisraeli elfu ine waliuawa kwenye uwanja wa vita.