1 Samuel 4:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, alipokuwa anakufa, wanawake waliokuwa wanamsaidia walimwambia, “Usiogope, maana umejifungua mtoto wa kiume.” Lakini yeye hakujibu neno, wala hakuwasikiliza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokuwa akifa, wanawake waliokuwa wanamhudumia wakamwambia, “Usiogope, umemzaa mwana wa kiume.” Lakini hakujibu wala kuweka maanani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, alipokuwa anakufa, wanawake waliokuwa wanamsaidia walimwambia, “Usiogope, maana umejifungua mtoto wa kiume.” Lakini yeye hakujibu neno, wala hakuwasikiliza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipokuwa akifa, wanawake waliokuwa wanamhudumia wakamwambia, “Usikate tamaa, umemzaa mwana.” Lakini hakujibu wala kuweka maanani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokuwa akifa, wanawake waliokuwa wanamhudumia wakamwambia, “Usikate tamaa, umemzaa mwana.” Lakini hakujibu wala kuweka maanani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na alipokuwa karibu kufa, wale wanawake waliokuwa wakimuhudumia wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto wa kiume. Lakini hakujibu, wala hakumtazama.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, alipokuwa anakufa, wanawake waliokuwa wanamsaidia walimwambia, “Usiogope, maana umejifungua mtoto wa kiume.” Lakini yeye hakujibu neno, wala hakuwasikiliza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, alipotaka kufa, wanawake waliomsimamia wakamwambia: Usiogope! Kwani umezaa mtoto wa kiume; lakini hakujibu neno, wala hakusikiliza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kwa sababu alikuwa karibu ya kufa, wanawake waliokuwa wanamuzalisha walimwambia: “Usiogope, maana umezaa mutoto mwanaume.” Lakini yeye hakujibu neno, wala hakuwasikiliza.