1 Samuel 4:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanajeshi walionusurika walipowasili kambini, wazee wa Israeli walisema, “Kwa nini Mwenyezi-Mungu amewaacha Wafilisti watushinde leo? Twendeni tukalilete sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu kutoka Shilo, ili aweze kwenda nasi vitani na kutuokoa kutoka na zetu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Askari waliporudi kambini, wazee wa Israeli wakawauliza, “Kwa nini Mwenyezi Mungu ameruhusu leo tushindwe mbele ya Wafilisti? Tuleteni Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu kutoka Shilo, ili lipate kwenda pamoja nasi, na kutuokoa kutoka mikono ya adui zetu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona Bwana ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la agano la Bwana toka Shilo hata huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanajeshi walionusurika walipowasili kambini, wazee wa Israeli walisema, “Kwa nini Mwenyezi-Mungu amewaacha Wafilisti watushinde leo? Twendeni tukalilete sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu kutoka Shilo, ili aweze kwenda nasi vitani na kutuokoa kutoka na zetu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Askari waliporudi kambini, wazee wa Israeli wakawauliza, “Kwa nini BWANA ameruhusu leo tushindwe mbele ya Wafilisti? Tulete Sanduku la Agano la BWANA kutoka Shilo, ili kwamba lipate kwenda pamoja nasi na kutuokoa kutoka mkono wa adui zetu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Askari waliporudi kambini, wazee wa Israeli wakawauliza, “Kwa nini bwana ameruhusu leo tushindwe mbele ya Wafilisti? Tuleteni Sanduku la Agano la bwana kutoka Shilo, ili lipate kwenda pamoja nasi, na kutuokoa kutoka mikono ya adui zetu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona BWANA ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la Agano la BWANA kutoka Shilo hadi huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanajeshi walionusurika walipowasili kambini, wazee wa Israeli walisema, “Kwa nini Mwenyezi-Mungu amewaacha Wafilisti watushinde leo? Twendeni tukalilete sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu kutoka Shilo, ili aweze kwenda nasi vitani na kutuokoa kutoka na zetu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu walipokuja kuingia makambini, wazee wa Waisiraeli wakasema: Sababu gani Bwana ametupiga leo machoni pao Wafilisti? Na tulichukue huko Silo Sanduku la Agano la Bwana, lije lituokoe mikononi mwa adui zetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona BWANA ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la agano la BWANA toka Shilo hata huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaskari walioponyoka walipofika kwenye kambi, wazee wa Israeli walisema: “Kwa nini Yawe amewaacha Wafilistini watushinde leo? Tuende tulilete Sanduku la Agano la Yawe kutoka Shilo, kusudi aweze kwenda nasi katika vita na kutuokoa kutoka waadui zetu.”