1 Samuel 5:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake asubuhi, watu wa mji wa Ashdodi walipoamka waliona sanamu ya Dagoni imeanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Mungu. Wakaisimamisha tena sanamu ya Dagoni na kuiweka tena mahali pake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la Bwana. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake asubuhi, watu wa mji wa Ashdodi walipoamka waliona sanamu ya Dagoni imeanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Mungu. Wakaisimamisha tena sanamu ya Dagoni na kuiweka tena mahali pake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la BWANA! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la bwana! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake asubuhi, watu wa mji wa Ashdodi walipoamka waliona sanamu ya Dagoni imeanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Mungu. Wakaisimamisha tena sanamu ya Dagoni na kuiweka tena mahali pake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake watu wa Asdodi walipoamka asubuhi wakamkuta Dagoni, akilala usoni chini mbele ya Sanduku la Bwana; wakamchukua Dagoni, wakamrudisha mahali pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake asubui, watu wa muji wa Asidodi walipoamuka waliona sanamu ya Dagoni imeanguka ikilalia uso chini mbele ya Sanduku la Mungu. Wakaisimamisha tena sanamu ya Dagoni na kuiweka tena pahali pake.