1 Samuel 5:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, kesho yake asubuhi walipoamka, waliona kuwa sanamu ya Dagoni imeanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu, kichwa, miguu na mikono ya sanamu hiyo, vyote vilikuwa vimekatika, vikawa vimelala chini kwenye kizingiti cha mlango. Kiwiliwili cha sanamu ya Dagoni ndicho tu kilikuwa kimebakia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini asubuhi iliyofuata, walipoamka kumbe, walimkuta Dagoni ameanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa, navyo vimelala kizingitini; ni kiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata walipoamka kesho yake asubuhi, kumbe! Dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la Bwana; na kichwa chake Dagoni na vitanga vya mikono yake vyote viwili vimekatika, vipo vimelala kizingitini; Dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, kesho yake asubuhi walipoamka, waliona kuwa sanamu ya Dagoni imeanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu, kichwa, miguu na mikono ya sanamu hiyo, vyote vilikuwa vimekatika, vikawa vimelala chini kwenye kizingiti cha mlango. Kiwiliwili cha sanamu ya Dagoni ndicho tu kilikuwa kimebakia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini asubuhi iliyofuata, walipoamka kumbe, walimkuta huyo Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la BWANA! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa navyo vimelala kizingitini, ni kiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini asubuhi iliyofuata, walipoamka kumbe, walimkuta huyo Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la bwana! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa navyo vimelala kizingitini, ni kiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata walipoamka kesho yake asubuhi, kumbe! Dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA; na kichwa chake Dagoni na vitanga vyote viwili vya mikono yake vimekatika, na kulazwa kizingitini; Dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, kesho yake asubuhi walipoamka, waliona kuwa sanamu ya Dagoni imeanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu, kichwa, miguu na mikono ya sanamu hiyo, vyote vilikuwa vimekatika, vikawa vimelala chini kwenye kizingiti cha mlango. Kiwiliwili cha sanamu ya Dagoni ndicho tu kilikuwa kimebakia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake walipoamka asubuhi wakamkuta Dagoni tena, akilala usoni chini mbele ya Sanduku la Bwana, nacho kichwa cha Dagoni na viganja vyote viwili vya mikono yake vilikuwa vimekatika, vilikuwa penye kizingiti, nao mwili ulikuwa umesalia peke yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata walipoamka kesho yake asubuhi, kumbe! Dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA; na kichwa chake Dagoni na vitanga vya mikono yake vyote viwili vimekatika, vipo vimelala kizingitini; Dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, kesho yake asubui walipoamuka, waliona kwamba sanamu ya Dagoni imeanguka uso chini mbele ya Sanduku la Yawe, kichwa, miguu na mikono ya sanamu hiyo, vyote vilikuwa vimekatika, vikakuwa vimelala chini kwenye kizingiti cha mulango. Kiwiliwili cha sanamu ya Dagoni ndicho tu kilikuwa kimebakia.