1 Samuel 5:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu aliwaadhibu vikali na kuwatisha watu wa Ashdodi. Aliwaadhibu, hata na majirani zao, kwa kuwaletea ugonjwa wa majipu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi na vijiji jirani, akaleta uharibifu juu yao na kuwatesa kwa majipu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mkono wa Bwana ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi, akawaharibu, akawapiga kwa majipu, huko Ashdodi na mipakani mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu aliwaadhibu vikali na kuwatisha watu wa Ashdodi. Aliwaadhibu, hata na majirani zao, kwa kuwaletea ugonjwa wa majipu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi na vijiji vya jirani akaleta uharibifu juu yao na kuwatesa kwa majipu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkono wa bwana ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi na vijiji jirani, akaleta uharibifu juu yao na kuwatesa kwa majipu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi, akawaangamiza, akawapiga kwa majipu, huko Ashdodi na mipakani mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu aliwaadhibu vikali na kuwatisha watu wa Ashdodi. Aliwaadhibu, hata na majirani zao, kwa kuwaletea ugonjwa wa majipu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkono wa Bwana ukawalemea watu wa Asdodi, akawaangamiza na kuwapiga kwa majipu mabaya waliokuwamo Asdodi namo katika mipaka yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi, akawaharibu, akawapiga kwa majipu, huko Ashdodi na mipakani mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe aliwaazibu vikali na kuwatisha watu wa Asidodi. Aliwaazibu, hata na wajirani zao, kwa kuwaletea ugonjwa wa majipu.