1 Samuel 6:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walawi walikuwa wameliteremsha sanduku la Mwenyezi-Mungu na lile kasha lenye vinyago vya dhahabu na kuviweka kwenye lile jiwe kubwa. Basi, siku hiyo watu wa Beth-shemeshi walitoa sadaka za kuteketezwa, na kumtolea tambiko Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walawi walilishusha Sanduku la Mwenyezi Mungu, pamoja na lile kasha lililokuwa na vile vitu vya dhahabu na kuviweka juu ya ule mwamba mkubwa. Siku ile watu wa Beth-Shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao Walawi walilishusha sanduku la Bwana, na lile kasha lililokuwa pamoja nalo, lenye vile vitu vya dhahabu; wakaviweka juu ya lile jiwe kubwa; nao watu wa Beth-shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja dhabihu siku iyo hiyo kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walawi walikuwa wameliteremsha sanduku la Mwenyezi-Mungu na lile kasha lenye vinyago vya dhahabu na kuviweka kwenye lile jiwe kubwa. Basi, siku hiyo watu wa Beth-shemeshi walitoa sadaka za kuteketezwa, na kumtolea tambiko Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walawi walilishusha Sanduku la BWANA, pamoja na lile kasha lililokuwa na vile vitu vya dhahabu na kuviweka juu ya ule mwamba mkubwa. Siku ile watu wa Beth-Shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walawi walilishusha Sanduku la bwana, pamoja na lile kasha lililokuwa na vile vitu vya dhahabu na kuviweka juu ya ule mwamba mkubwa. Siku ile watu wa Beth-Shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao Walawi walilishusha sanduku la BWANA, na lile kasha lililokuwa pamoja nalo, lenye vile vitu vya dhahabu; wakaviweka juu ya lile jiwe kubwa; nao watu wa Beth-shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja dhabihu siku hiyo hiyo kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walawi walikuwa wameliteremsha sanduku la Mwenyezi-Mungu na lile kasha lenye vinyago vya dhahabu na kuviweka kwenye lile jiwe kubwa. Basi, siku hiyo watu wa Beth-shemeshi walitoa sadaka za kuteketezwa, na kumtolea tambiko Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao Walawi wakalishusha Sanduku la Bwana na kile kisanduku kilichowekwa pamoja nalo, kilichotiwa vile vyombo vya dhahabu, wakaliweka juu ya hilo jiwe kubwa. Kisha watu wa Beti-Semesi wakatoa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, wakachinja nazo ng'ombe nyingine za tambiko siku ileile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao Walawi walilishusha sanduku la BWANA, na lile kasha lililokuwa pamoja nalo, lenye vile vitu vya dhahabu; wakaviweka juu ya lile jiwe kubwa; nao watu wa Beth-shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja dhabihu siku iyo hiyo kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walawi walikuwa wameliteremusha Sanduku la Yawe na kile kibweta chenye sanamu za zahabu na kuziweka kwenye lile jiwe kubwa. Basi, siku hiyo watu wa Beti-Semesi walitoa sadaka za kuteketezwa, na kumutolea Yawe sadaka.