1 Samuel 6:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipeleka pia vinyago vitano vya dhahabu vya panya kulingana na hesabu ya miji yote ya Wafilisti iliyotawaliwa na wakuu watano wa Wafilisti. Miji hiyo ilikuwa yenye ngome na vijiji ambavyo havikuzungushiwa kuta. Lile jiwe kubwa kwenye shamba la Yoshua wa Beth-shemeshi, mahali ambapo walilipeleka sanduku la Mwenyezi-Mungu, ni ushahidi wa tukio hilo hadi leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nayo hesabu ya wale panya wa dhahabu ilikuwa kulingana na idadi ya miji ya Wafilisti ya watawala watano wa Wafilisti: miji yao yenye ngome, pamoja na vijiji vya miji hiyo. Ule mwamba mkubwa, ambao juu yake waliliweka lile Sanduku la Mwenyezi Mungu, ni ushahidi hadi leo katika shamba la Yoshua wa Beth-Shemeshi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na panya wa dhahabu, kwa idadi ya miji yote ya Wafilisti, milki zao wale mashehe watano, miji yenye maboma na vijiji vya mashamba pia. Nalo lile jiwe kubwa, ambalo juu yake waliliweka sanduku la Bwana, liko hata hivi leo hapo kondeni pa Yoshua wa Beth-shemeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipeleka pia vinyago vitano vya dhahabu vya panya kulingana na hesabu ya miji yote ya Wafilisti iliyotawaliwa na wakuu watano wa Wafilisti. Miji hiyo ilikuwa yenye ngome na vijiji ambavyo havikuzungushiwa kuta. Lile jiwe kubwa kwenye shamba la Yoshua wa Beth-shemeshi, mahali ambapo walilipeleka sanduku la Mwenyezi-Mungu, ni ushahidi wa tukio hilo hadi leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nayo hesabu ya wale panya wa dhahabu ilikuwa kulingana na idadi ya miji ya Wafilisti ya watawala watano wa Wafilisti, na miji yao iliyozungukwa na maboma pamoja na vijiji vya nchi yao. Ule mwamba mkubwa, ambao juu yake waliliweka lile Sanduku la BWANA, ni ushahidi hadi leo katika shamba la Yoshua wa Beth-Shemeshi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nayo hesabu ya wale panya wa dhahabu ilikuwa kulingana na idadi ya miji ya Wafilisti ya watawala watano wa Wafilisti: miji yao iliyozungukwa na maboma, pamoja na vijiji vya miji hiyo. Ule mwamba mkubwa, ambao juu yake waliliweka lile Sanduku la bwana, ni ushahidi hadi leo katika shamba la Yoshua wa Beth-Shemeshi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na panya wa dhahabu, kwa idadi ya miji yote ya Wafilisti, milki zao wale wakuu watano, miji yenye maboma na vijiji vya mashamba pia. Nalo lile jiwe kubwa, ambalo juu yake waliliweka sanduku la BWANA, liko hata hivi leo hapo kondeni pa Yoshua wa Beth-shemeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipeleka pia vinyago vitano vya dhahabu vya panya kulingana na hesabu ya miji yote ya Wafilisti iliyotawaliwa na wakuu watano wa Wafilisti. Miji hiyo ilikuwa yenye ngome na vijiji ambavyo havikuzungushiwa kuta. Lile jiwe kubwa kwenye shamba la Yoshua wa Beth-shemeshi, mahali ambapo walilipeleka sanduku la Mwenyezi-Mungu, ni ushahidi wa tukio hilo hadi leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo panya za dhahabu hesabu yao ilikuwa sawa na hesabu ya miji yote ya Wafilisti ya hao wakuu watano, ya miji yenye maboma na ya vijiji vya shambani. Hivi vinashuhudiwa na lile jiwe kubwa, ambalo wameliweka Sanduku la Bwana juu yake, nalo liko hata siku hii ya leo shambani kwa Yosua huko Beti-Semesi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na panya wa dhahabu, kwa idadi ya miji yote ya Wafilisti, milki zao wale mashehe watano, miji yenye maboma na vijiji vya mashamba pia. Nalo lile jiwe kubwa, ambalo juu yake waliliweka sanduku la BWANA, liko hata hivi leo hapo kondeni pa Yoshua wa Beth-shemeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipeleka vilevile sanamu za zahabu za panya kulingana na hesabu ya miji yote ya Wafilistini iliyotawaliwa na wakubwa watano wa Wafilistini. Miji hiyo ilikuwa yenye kuzungukwa na kuta na vijiji ambavyo havikuzungushiwa kuta. Lile jiwe kubwa kwenye shamba la Yoshua wa Beti-Semesi, pahali ambapo walilipeleka Sanduku la Yawe, ni ushuhuda wa tukio hilo mpaka leo.