1 Samuel 6:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu aliwaua wakazi sabini wa mji wa Beth-shemeshi, kwa sababu waliangalia ndani ya sanduku lake. Watu waliomboleza kwa sababu Mwenyezi-Mungu alikuwa amefanya mauaji makubwa miongoni mwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mungu aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-Shemeshi, akiwaua watu sabini miongoni mwao kwa sababu walichungulia ndani ya Sanduku la Mwenyezi Mungu. Watu wakaomboleza kwa sababu ya pigo zito kutoka kwa Mwenyezi Mungu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Bwana aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-shemeshi, kwa sababu wamechungulia ndani ya hilo sanduku la Bwana, wapata watu sabini, na watu hamsini elfu; nao watu wakalalamika, kwa kuwa Bwana amewapiga watu kwa uuaji mkuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu aliwaua wakazi sabini wa mji wa Beth-shemeshi, kwa sababu waliangalia ndani ya sanduku lake. Watu waliomboleza kwa sababu Mwenyezi-Mungu alikuwa amefanya mauaji makubwa miongoni mwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mungu aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-Shemeshi, akiwaua watu sabini miongoni mwao kwa sababu walichungulia ndani ya Sanduku la BWANA. Watu wakaomboleza kwa sababu ya pigo zito kutoka kwa BWANA,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Mungu aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-Shemeshi, akiwaua watu sabini miongoni mwao kwa sababu walichungulia ndani ya Sanduku la bwana. Watu wakaomboleza kwa sababu ya pigo zito kutoka kwa bwana,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi BWANA aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-shemeshi, kwa sababu wamechungulia ndani ya hilo sanduku la BWANA, wapata watu sabini, na watu elfu hamsini; nao watu wakalalamika, kwa kuwa BWANA amewapiga watu kwa uuaji mkuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu aliwaua wakazi sabini wa mji wa Beth-shemeshi, kwa sababu waliangalia ndani ya sanduku lake. Watu waliomboleza kwa sababu Mwenyezi-Mungu alikuwa amefanya mauaji makubwa miongoni mwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
(Bwana) akawapiga watu wa Beti-Semesi, kwa kuwa wamechungulia Sandukuni mwa Bwana, akapiga kwao watu 70, tena watu 50000; ndipo, watu walipolia sana, kwa kuwa Bwana amewapiga wa kwao pigo kubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi BWANA aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-shemeshi, kwa sababu wamechungulia ndani ya hilo sanduku la BWANA, wapata watu sabini, na watu hamsini elfu; nao watu wakalalamika, kwa kuwa BWANA amewapiga watu kwa uuaji mkuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe aliwaua wakaaji makumi saba wa muji wa Beti-Semesi, kwa sababu waliangalia ndani ya Sanduku lake. Watu waliomboleza kwa sababu Yawe alikuwa amefanya mauaji makubwa kati yao.