1 Samuel 6:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lazima mfanye vinyago vya majipu na vinyago vya panya wenu, vitu ambavyo vinaangamiza nchi yenu. Ni lazima mumpe heshima Mungu wa Israeli. Labda ataacha kuwaadhibu, nyinyi wenyewe, miungu yenu na nchi yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tengenezeni mifano ya majipu na ya panya wale wanaoharibu nchi yenu, nanyi mtukuzeni Mungu wa Israeli. Labda ataondoa mkono wake kutoka kwenu na kwa miungu yenu na nchi yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo mtafanyiza sanamu za majipu yenu, na sanamu za panya wenu waiharibuo nchi; nanyi mtamtukuza huyo Mungu wa Israeli; huenda ataupunguza uzito wa mkono wake juu yenu, na juu ya miungu yenu, na juu ya nchi yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lazima mfanye vinyago vya majipu na vinyago vya panya wenu, vitu ambavyo vinaangamiza nchi yenu. Ni lazima mumpe heshima Mungu wa Israeli. Labda ataacha kuwaadhibu, nyinyi wenyewe, miungu yenu na nchi yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tengenezeni mifano ya majipu na ya mapanya wale wanaoharibu nchi yenu, nanyi mheshimuni Mungu wa Israeli. Labda ataondoa mkono wake kutoka kwenu na kwa miungu yenu na nchi yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tengenezeni mifano ya majipu na ya panya wale wanaoharibu nchi yenu, nanyi mheshimuni Mungu wa Israeli. Labda ataondoa mkono wake kutoka kwenu na kwa miungu yenu na nchi yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo mtafanya sanamu za majipu yenu, na sanamu za panya wenu wanaoiharibu nchi; nanyi mtamtukuza huyo Mungu wa Israeli; huenda ataupunguza uzito wa mkono wake juu yenu, na juu ya miungu yenu, na juu ya nchi yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lazima mfanye vinyago vya majipu na vinyago vya panya wenu, vitu ambavyo vinaangamiza nchi yenu. Ni lazima mumpe heshima Mungu wa Israeli. Labda ataacha kuwaadhibu, nyinyi wenyewe, miungu yenu na nchi yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ifanyeni hiyo mifano ya majipu yenu mabaya na ya panya wenu wanaoiangamiza nchi hii, kisha mmpe Mungu wa Waisiraeli macheo, labda ataugeuza mkono wake kuwa mwepesi kwenu na kwa miungu yenu na katika nchi yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo mtafanyiza sanamu za majipu yenu, na sanamu za panya wenu waiharibuo nchi; nanyi mtamtukuza huyo Mungu wa Israeli; huenda ataupunguza uzito wa mkono wake juu yenu, na juu ya miungu yenu, na juu ya nchi yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mufanye sanamu zenu za majipu na sanamu za panya, vitu ambavyo vinaangamiza inchi yenu, nanyi mutamutukuza Mungu wa Israeli. Labda ataacha kuwaazibu ninyi wenyewe, miungu yenu na inchi yenu.