1 Samuel 6:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, tayarisheni gari jipya na ng'ombe wawili wakamuliwao ambao bado hawajafungwa nira; wafungeni kwenye gari hilo lakini ndama wao wasiende pamoja nao, ila wabaki zizini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sasa basi, wekeni gari jipya la kukokotwa pamoja na ng’ombe wawili ambao wamezaa lakini ambao kamwe hawajafungwa nira. Fungieni hao ng’ombe hilo gari, lakini ondoeni ndama wao na mwaweke zizini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa jifanyizieni gari jipya, mtwae na ng'ombe wake wawili wakamwao, ambao hawajafungwa nira, nanyi mkawafunge hao ng'ombe garini, na kuwaondoa ndama zao na kuwatia zizini;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, tayarisheni gari jipya na ng'ombe wawili wakamuliwao ambao bado hawajafungwa nira; wafungeni kwenye gari hilo lakini ndama wao wasiende pamoja nao, ila wabaki zizini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sasa basi, wekeni gari jipya la kukokotwa pamoja na ng'ombe wawili ambao wamezaa lakini ambao kamwe hawajafungwa nira. Fungieni hao ng'ombe hilo gari, lakini ondoeni ndama wao na muwaweke zizini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sasa basi, wekeni gari jipya la kukokotwa pamoja na ng’ombe wawili ambao wamezaa lakini ambao kamwe hawajafungwa nira. Fungieni hao ng’ombe hilo gari, lakini ondoeni ndama wao na mwaweke zizini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa jifanyieni gari jipya, mtwae na ng'ombe wake wawili wakamuliwao, ambao hawajafungwa nira, nanyi mkawafunge hao ng'ombe garini, na kuwaondoa ndama wao na kuwatia zizini;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, tayarisheni gari jipya na ng'ombe wawili wakamuliwao ambao bado hawajafungwa nira; wafungeni kwenye gari hilo lakini ndama wao wasiende pamoja nao, ila wabaki zizini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa tengenezeni gari jipya moja, tena chukueni ng'ombe wawili wanyonyeshao, wasiobandikiwa bado mti wa kuvutia gari! Kisha wafungeni hao ng'ombe penye hilo gari, miwaondoa watoto wao kwao na kuwarudisha nyumbani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa jifanyizieni gari jipya, mtwae na ng’ombe wake wawili wakamwao, ambao hawajafungwa nira, nanyi mkawafunge hao ng’ombe garini, na kuwaondoa ndama zao na kuwatia zizini;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mutayarishe gari jipya na ngombe wawili wenye kunyonyesha ambao bado hawajafungwa nira. Muwafunge kwenye gari hilo lakini vitoto vyao visiende pamoja nao, lakini vibaki katika zizi.