1 Samuel 7:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, watu wa Kiriath-yearimu wakaenda na kulichukua sanduku la Mwenyezi-Mungu, wakalipeleka nyumbani kwa Abinadabu, aliyeishi milimani. Wakamweka wakfu mtoto wake wa kiume aliyeitwa Eleazari ili alitunze sanduku hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wanaume wa Kiriath-Yearimu wakaja na kulichukua Sanduku la Mwenyezi Mungu. Wakalipeleka katika nyumba ya Abinadabu kilimani, na kumweka Eleazari mwanawe wakfu kulichunga Sanduku la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao watu wa Kiriath-yearimu wakaja, wakalichukua sanduku la Bwana, wakalileta ndani ya nyumba ya Abinadabu huko kilimani, nao wakamtenga Eleazari, mwanawe, ili alilinde sanduku la Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, watu wa Kiriath-yearimu wakaenda na kulichukua sanduku la Mwenyezi-Mungu, wakalipeleka nyumbani kwa Abinadabu, aliyeishi milimani. Wakamweka wakfu mtoto wake wa kiume aliyeitwa Eleazari ili alitunze sanduku hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watu wa Kiriath-Yearimu wakaja na kulichukua Sanduku la BWANA. Wakalipeleka katika nyumba ya Abinadabu juu kilimani na kumweka Eleazari mwanawe wakfu kulichunga Sanduku la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watu wa Kiriath-Yearimu wakaja na kulichukua Sanduku la bwana. Wakalipeleka katika nyumba ya Abinadabu juu kilimani na kumweka Eleazari mwanawe wakfu kulichunga Sanduku la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao watu wa Kiriath-yearimu wakaja, wakalichukua sanduku la BWANA, wakalipeleka ndani ya nyumba ya Abinadabu huko kilimani, nao wakamtenga Eleazari, mwanawe, ili alilinde sanduku la BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, watu wa Kiriath-yearimu wakaenda na kulichukua sanduku la Mwenyezi-Mungu, wakalipeleka nyumbani kwa Abinadabu, aliyeishi milimani. Wakamweka wakfu mtoto wake wa kiume aliyeitwa Eleazari ili alitunze sanduku hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wa Kiriati-Yearimu wakaja, wakalichukua Sanduku la Bwana kwao, wakaliingiza nyumbani mwa Abinadabu kilimani juu, naye mwanawe Elazari wakamweua, aliangalie Sanduku la Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao watu wa Kiriath-yearimu wakaja, wakalichukua sanduku la BWANA, wakalileta ndani ya nyumba ya Abinadabu huko kilimani, nao wakamtenga Eleazari, mwanawe, ili alilinde sanduku la BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, watu wa Kiriati-Yearimu wakaenda na kulikamata Sanduku la Yawe, wakalipeleka katika nyumba ya Abinadabu, aliyeishi kwenye milima. Wakamutakasa mwana wake aliyeitwa Eleazari kusudi alitunze Sanduku hilo.