1 Samuel 7:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tangu sanduku la Mwenyezi-Mungu lipelekwe mjini Kiriath-yearimu muda mrefu ulipita, miaka ishirini hivi. Wakati huo Waisraeli wote walimlilia Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sanduku la Mwenyezi Mungu lilibakia huko Kiriath-Yearimu kwa muda mrefu, jumla ya miaka ishirini. Nao watu wote wa Israeli wakamrudia Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, tangu siku hiyo ambayo sanduku lilikaa Kiriath-yearimu wakati ulikuwa mwingi; kwa maana ulikuwa miaka ishirini; na nyumba yote ya Israeli wakamwombolezea Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tangu sanduku la Mwenyezi-Mungu lipelekwe mjini Kiriath-yearimu muda mrefu ulipita, miaka ishirini hivi. Wakati huo Waisraeli wote walimlilia Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sanduku la BWANA lilibakia huko Kiriath-Yearimu kwa muda mrefu, yaani jumla ya miaka ishirini, nao watu wa Israeli wakaomboleza na kumtafuta BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sanduku la bwana lilibakia huko Kiriath-Yearimu kwa muda mrefu, yaani jumla ya miaka ishirini, nao watu wa Israeli wakaomboleza na kumtafuta bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, tangu sanduku lipelekwe Kiriath-yearimu, muda mrefu ulipita; maana ulikuwa miaka ishirini; na nyumba yote ya Waisraeli wakamwombolezea BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tangu sanduku la Mwenyezi-Mungu lipelekwe mjini Kiriath-yearimu muda mrefu ulipita, miaka ishirini hivi. Wakati huo Waisraeli wote walimlilia Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tangu siku hiyo, Sanduku la Bwana lilipokuja kukaa Kiriati-Yearimu, siku zikapita nyingi, zikawa miaka 20. Kisha mlango wote wa Waisiraeli wakageuka kumfuata Bwana na kumlilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, tangu siku hiyo ambayo sanduku lilikaa Kiriath-yearimu wakati ulikuwa mwingi; kwa maana ulikuwa miaka ishirini; na nyumba yote ya Israeli wakamwombolezea BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tangu Sanduku la Yawe lilipopelekwa katika muji wa Kiriati-Yearimu, kulipita muda murefu, miaka makumi mbili hivi. Wakati huo Waisraeli wote walimulilia Yawe.