1 Samuel 7:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Samueli akawaambia Waisraeli, “Kama mnamrudia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wenu wote, ni lazima mwondoe kati yenu miungu ya kigeni na sanamu za Ashtarothi. Mwelekeeni Mwenyezi-Mungu kwa moyo wote, na kumtumikia yeye peke yake; naye atawaokoa kutoka mikononi mwa Wafilisti.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, “Ikiwa mtamrudia Mwenyezi Mungu kwa mioyo yenu yote, basi iacheni miungu migeni na Maashtorethi, na kujitoa wenyewe kwa Mwenyezi Mungu na kumtumikia yeye peke yake, naye atawaokoa ninyi kutoka kwa mkono wa Wafilisti.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia Bwana kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee Bwana mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Samueli akawaambia Waisraeli, “Kama mnamrudia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wenu wote, ni lazima mwondoe kati yenu miungu ya kigeni na sanamu za Ashtarothi. Mwelekeeni Mwenyezi-Mungu kwa moyo wote, na kumtumikia yeye peke yake; naye atawaokoa kutoka mikononi mwa Wafilisti.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, “Ikiwa mtamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi iacheni miungu migeni na Maashtorethi na kujitoa wenyewe kwa BWANA na kumtumikia yeye peke yake, naye atawaokoa ninyi na mkono wa Wafilisti.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, “Ikiwa mtamrudia bwana kwa mioyo yenu yote, basi iacheni miungu migeni na Maashtorethi na kujitoa wenyewe kwa bwana na kumtumikia yeye peke yake, naye atawaokoa ninyi na mkono wa Wafilisti.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamwelekezee BWANA mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Samueli akawaambia Waisraeli, “Kama mnamrudia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wenu wote, ni lazima mwondoe kati yenu miungu ya kigeni na sanamu za Ashtarothi. Mwelekeeni Mwenyezi-Mungu kwa moyo wote, na kumtumikia yeye peke yake; naye atawaokoa kutoka mikononi mwa Wafilisti.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Samweli alipouambia mlango wote wa Waisiraeli kwamba: Ninyi mkimgeukia Bwana kwa mioyo yote, iondoeni miungu migeni kwenu pamoja na Maastaroti! Kisha ielekezeni mioyo yenu kwake Bwana na kumtumikia yeye peke yake! Ndivyo, atakavyowaponya mikononi mwa wafilisti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee BWANA mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Samweli akawaambia Waisraeli: “Kama munamurudilia Yawe kwa moyo wenu wote, basi mutupilie mbali miungu ya kigeni na sanamu za Astaroti. Muelekeze mioyo yenu kwa Yawe, na kumutumikia yeye peke yake; naye atawaokoa kutoka katika mikono ya Wafilistini.”