1 Samuel 8:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Samueli aliwaambia, “Hivi ndivyo mfalme wenu atakayewatawala atakavyowatendea: Watoto wenu wa kiume atawafanya wawe waendeshaji wa magari yake, na wengine kuwa wapandafarasi wake, na wengine watapiga mbio mbele ya magari yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Samueli aliwaambia, “Hivi ndivyo mfalme wenu atakayewatawala atakavyowatendea: watoto wenu wa kiume atawafanya wawe waendeshaji wa magari yake, na wengine kuwa wapandafarasi wake, na wengine watapiga mbio mbele ya magari yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Mfalme atakayewatawala ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, katika magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Samueli aliwaambia, “Hivi ndivyo mfalme wenu atakayewatawala atakavyowatendea: Watoto wenu wa kiume atawafanya wawe waendeshaji wa magari yake, na wengine kuwa wapandafarasi wake, na wengine watapiga mbio mbele ya magari yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akisema: Hii ndiyo haki yake mfalme atakayewatawala: atawachukua wana wenu wa kiume, awaweke katika magari yake wa kuyaendesha, wengine atawapandisha farasi, wengine atawaweka kuyatangulia magari yake kwa kupiga mbio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Samweli aliwaambia: “Hivi ndivyo mufalme wenu atakayewatawala atakavyowatendea: wana wenu atawafanya wakuwe waendeshaji wa magari yake, na wengine kuwa waaskari wapanda-farasi wake, na wengine watapiga mbio mbele ya magari yake.