1 Samuel 9:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara mtakapoingia mjini, mtamkuta kabla hajaenda mahali pa ibada mlimani ili kula. Maana watu hawatakula mpaka kwanza yeye abariki tambiko. Baadaye wale walioalikwa watakula. Hivyo nendeni haraka; mtakutana naye mara.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara tu mwingiapo mjini, mtamkuta kabla hajapanda kwenda mahali pa juu pa kuabudia ili kula. Watu hawataanza kula hadi atakapofika, kwa sababu ni lazima kwanza yeye abariki dhabihu, ndipo wale walioalikwa watakapokula. Pandeni sasa, mtamkuta kwa wakati huu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mkiingia mjini tu, mara mtamwona, kabla hajakwea kwenda mahali pa juu ale chakula; maana, watu hawatakula hata yeye atakapokuja; kwa sababu yeye ndiye anayeibarikia dhabihu; kisha hao watu walioalikwa hula. Basi, kweeni sasa; maana wakati huu ndio mtakapomwona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara mtakapoingia mjini, mtamkuta kabla hajaenda mahali pa ibada mlimani ili kula. Maana watu hawatakula mpaka kwanza yeye abariki tambiko. Baadaye wale walioalikwa watakula. Hivyo nendeni haraka; mtakutana naye mara.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara tu mwingiapo mjini, mtamkuta kabla hajapanda kwenda mahali pa juu kula. Watu hawataanza kula mpaka atakapofika kwa sababu ni lazima kwanza yeye abariki dhabihu, ndipo wale walioalikwa watakapokula. Pandeni sasa, mtamkuta kwa wakati huu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara tu mwingiapo mjini, mtamkuta kabla hajapanda kwenda mahali pa juu kula. Watu hawataanza kula mpaka atakapofika kwa sababu ni lazima kwanza yeye abariki dhabihu, ndipo wale walioalikwa watakapokula. Pandeni sasa, mtamkuta kwa wakati huu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mkiingia mjini tu, mara mtamwona, kabla hajakwea kwenda mahali pa juu ale chakula; maana, watu hawatakula hadi yeye atakapokuja; kwa sababu yeye ndiye anayeibariki dhabihu; ndipo hao watu walioalikwa hula. Basi, kweeni sasa; maana wakati huu ndio mtakapomwona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara mtakapoingia mjini, mtamkuta kabla hajaenda mahali pa ibada mlimani ili kula. Maana watu hawatakula mpaka kwanza yeye abariki tambiko. Baadaye wale walioalikwa watakula. Hivyo nendeni haraka; mtakutana naye mara.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtakapoingia mjini, mtamkuta, hajapanda kilimani kula, kwani watu hawali, mpaka aje, kwani yeye kwanza sharti aibariki ng'ombe ya tambiko, kisha waalikwao hula. Sasa pandeni! Kwani siku kama hii ya leo mtamwona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mkiingia mjini tu, mara mtamwona, kabla hajakwea kwenda mahali pa juu ale chakula; maana, watu hawatakula hata yeye atakapokuja; kwa sababu yeye ndiye anayeibarikia dhabihu; kisha hao watu walioalikwa hula. Basi, kweeni sasa; maana wakati huu ndio mtakapomwona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara moja mutakapoingia katika muji, mutamukuta mbele hajakwenda kwenye nafasi ya ibada kwenye mulima kwa kula. Maana watu hawatakula mpaka kwanza yeye abariki sadaka. Kisha wale walioalikwa watakula. Hivyo muende haraka; mutakutana naye sasa hivi.”