1 Samuel 9:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mpishi akaenda akaleta paja na sehemu ya nyama iliyokuwa upande wa juu wa paja hilo na kuviweka mbele ya Shauli. Ndipo Samueli akamwambia Shauli, “Tazama kile ulichowekewa; sasa kimewekwa mbele yako. Sasa ule kwa sababu kimewekwa kwa ajili yako ili upate kula pamoja na wageni.” Hivyo, Shauli akala pamoja na Samueli siku hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo mpishi akachukua mguu pamoja na kile kilichokuwa juu yake akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, “Hiki ndicho ambacho kimewekwa kwa ajili yako. Ule, kwa sababu kilitengwa kwa ajili yako kwa tukio hili, tangu niliposema, ‘Nimewaalika wageni.’ ” Naye Sauli akala pamoja na Samweli siku ile.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mpishi akatwaa paja, na nyama iliyokuwa juu yake, akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, Iliyowekwa akiba ndiyo hiyo! Iweke mbele yako ule, kwa sababu umewekewa hiyo wewe hata wakati uliokusudiwa, maana nalisema, Nimewaalika watu. Basi Sauli akala pamoja na Samweli siku hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mpishi akaenda akaleta paja na sehemu ya nyama iliyokuwa upande wa juu wa paja hilo na kuviweka mbele ya Shauli. Ndipo Samueli akamwambia Shauli, “Tazama kile ulichowekewa; sasa kimewekwa mbele yako. Sasa ule kwa sababu kimewekwa kwa ajili yako ili upate kula pamoja na wageni.” Hivyo, Shauli akala pamoja na Samueli siku hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo mpishi akachukua mguu pamoja na kile kilichokuwa juu yake akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, “Hiki ndicho ambacho kimewekwa kwa ajili yako. Ule, kwa sababu kilitengwa kwa ajili yako kwa tukio hili, tangu niliposema, ‘Nimewaalika wageni.’ ” Naye Sauli akala pamoja na Samweli siku ile.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo mpishi akachukua mguu pamoja na kile kilichokuwa juu yake akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, “Hiki ndicho ambacho kimewekwa kwa ajili yako. Ule, kwa sababu kilitengwa kwa ajili yako kwa tukio hili, tangu niliposema, ‘Nimewaalika wageni.’ ” Naye Sauli akala pamoja na Samweli siku ile.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mpishi akatwaa paja, na nyama iliyokuwa juu yake, akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, Iliyowekwa kando ndiyo hiyo! Iweke mbele yako ule, kwa sababu umewekewa hiyo wewe hadi wakati uliokusudiwa, maana nilisema, Nimewaalika watu. Basi Sauli akala pamoja na Samweli siku hiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mpishi akaenda akaleta paja na sehemu ya nyama iliyokuwa upande wa juu wa paja hilo na kuviweka mbele ya Shauli. Ndipo Samueli akamwambia Shauli, “Tazama kile ulichowekewa; sasa kimewekwa mbele yako. Sasa ule kwa sababu kimewekwa kwa ajili yako ili upate kula pamoja na wageni.” Hivyo, Shauli akala pamoja na Samueli siku hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mpishi akachukua paja pamoja na nyama zilizoshikana nalo, akamwandalia Sauli. Samweli akamwambia Sauli: Tazama iliyosazwa! Jiandalie, ule! Kwani niliposema: Nimewaalika watu, umewekewa nyama hii kuwa ya saa hiihii. Basi, siku hiyo Sauli akala pamoja na Samweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mpishi akatwaa paja, na nyama iliyokuwa juu yake, akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, Iliyowekwa akiba ndiyo hiyo! Iweke mbele yako ule, kwa sababu umewekewa hiyo wewe hata wakati uliokusudiwa, maana nalisema, Nimewaalika watu. Basi Sauli akala pamoja na Samweli siku hiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mupishi akaenda akaleta paja na sehemu ya nyama iliyokuwa upande wa juu wa paja hilo na kuviweka mbele ya Saulo. Halafu Samweli akamwambia Saulo: “Angalia kile ulichowekewa; sasa kimewekwa mbele yako. Sasa ukule kwa sababu kimewekwa kwa ajili yako kusudi upate kula pamoja na wageni.” Hivyo, Saulo akakula pamoja na Samweli siku hiyo.