1 Samuel 9:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliporudi mjini kutoka mahali pa juu pa ibada, Shauli alitandikiwa kitanda kwenye paa la nyumba, akalala huko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kushuka kutoka mahali pa juu pa kuabudia na kufika mjini, Samweli alizungumza na Sauli juu ya dari ya nyumba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata waliposhuka kutoka mahali pa juu na kufika mjini, akaongea na Sauli darini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliporudi mjini kutoka mahali pa juu pa ibada, Shauli alitandikiwa kitanda kwenye paa la nyumba, akalala huko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kushuka kutoka mahali pa juu na kufika mjini, Samweli alizungumza na Sauli juu ya dari ya nyumba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kushuka kutoka mahali pa juu na kufika mjini, Samweli alizungumza na Sauli juu ya dari ya nyumba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata waliposhuka kutoka mahali pa juu na kufika mjini, akaongea na Sauli darini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliporudi mjini kutoka mahali pa juu pa ibada, Shauli alitandikiwa kitanda kwenye paa la nyumba, akalala huko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakatelemka wakitoka kilimani pa kutambikia kwenda mjini, naye Samweli akaja kuongea na Sauli darini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata waliposhuka kutoka mahali pa juu na kufika mjini, akaongea na Sauli darini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waliporudi katika muji kutoka kwenye nafasi ya ibada juu ya mulima, alizungumuza na Saulo juu ya dari. Na Saulo akalala kule.