1 Samuel 9:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipofika mwisho wa mji, Samueli akamwambia Shauli, “Mwambie huyo kijana atangulie mbele yetu.” Kijana alipokwisha ondoka, Samueli akaendelea kusema, “Ngoja kidogo, nami nitakufunulia yale aliyosema Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokuwa wakiteremka kuelekea mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, “Mwambie mtumishi atangulie mbele yetu.” Naye mtumishi akafanya hivyo. “Subiri hapa kidogo ili nipate kukupa ujumbe kutoka kwa Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata walipokuwa wakishuka mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipofika mwisho wa mji, Samueli akamwambia Shauli, “Mwambie huyo kijana atangulie mbele yetu.” Kijana alipokwisha ondoka, Samueli akaendelea kusema, “Ngoja kidogo, nami nitakufunulia yale aliyosema Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata walipokuwa wakitelemka kuelekea mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, “Mwambie mtumishi atangulie mbele yetu.” Naye mtumishi akafanya hivyo. “Lakini subiri hapa kwa kitambo kidogo, ili nipate kukupa ujumbe kutoka kwa Mungu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata walipokuwa wakiteremka kuelekea mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, “Mwambie mtumishi atangulie mbele yetu.” Naye mtumishi akafanya hivyo. “Lakini subiri hapa kwa kitambo kidogo, ili nipate kukupa ujumbe kutoka kwa Mungu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata walipokuwa wakishuka kuelekea viunga vya mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atutangulie, naye akitangulia, wewe nawe simama hapa kwa muda, ili nikuambie neno la Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipofika mwisho wa mji, Samueli akamwambia Shauli, “Mwambie huyo kijana atangulie mbele yetu.” Kijana alipokwisha ondoka, Samueli akaendelea kusema, “Ngoja kidogo, nami nitakufunulia yale aliyosema Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipotelemka, wafike mwishoni kwa mji, Samweli akamwambia Sauli: Mwambie kijana huyu, apite kwenda mbele yetu! Alipopita kwenda mbele, akasema: Lakini wewe simama sasa, nikuambie neno la Mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata walipokuwa wakishuka mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipofika mwisho wa muji, Samweli akamwambia Saulo: “Umwambie yule kijana atangulie mbele yetu.” Kijana alipokwisha ondoka, Samweli akaendelea kusema: “Ngoja kidogo, nami nitakufunulia yale Mungu aliyosema.”