1 Samuel 9:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipofika kwenye nchi ya Sufu, Shauli alimwambia mtumishi wake, “Turudi nyumbani, la sivyo baba yangu ataacha kufikiria juu ya punda, na badala yake atakuwa na wasiwasi juu yetu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipofika sehemu ya Sufu, Sauli akamwambia mtumishi aliyekuwa pamoja naye, “Njoo turudi, au baba yangu ataacha kufikiria kuhusu punda na kuanza kufadhaika kutuhusu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata walipofika nchi ya Sufu, Sauli akamwambia yule mtumishi aliyefuatana naye, Haya, na turudi, baba yangu asije akaacha kufikiri habari za punda akatufikiri sisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipofika kwenye nchi ya Sufu, Shauli alimwambia mtumishi wake, “Turudi nyumbani, la sivyo baba yangu ataacha kufikiria juu ya punda, na badala yake atakuwa na wasiwasi juu yetu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipofika sehemu ya Sufu, Sauli akamwambia mtumishi aliyekuwa pamoja naye, “Njoo, sisi na turudi, au baba yangu ataacha kufikiria juu ya punda na kuanza kufadhaika kuhusu sisi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipofika sehemu ya Sufu, Sauli akamwambia mtumishi aliyekuwa pamoja naye, “Njoo, sisi na turudi, au baba yangu ataacha kufikiria juu ya punda na kuanza kufadhaika kutuhusu sisi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walipofika katika nchi ya Sufu, Sauli akamwambia yule mtumishi aliyefuatana naye, Hebu turudi, baba yangu asije akaacha kufikiri habari za punda akatufikiri sisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipofika kwenye nchi ya Sufu, Shauli alimwambia mtumishi wake, “Turudi nyumbani, la sivyo baba yangu ataacha kufikiria juu ya punda, na badala yake atakuwa na wasiwasi juu yetu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakaingia katika nchi ya Sufu; ndipo, Sauli alipomwambia yule kijana, aliyekuwa naye: Haya! Na turudi, baba asiwaache wale punda, akatuhangaikia sisi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata walipofika nchi ya Sufu, Sauli akamwambia yule mtumishi aliyefuatana naye, Haya, na turudi, baba yangu asije akaacha kufikiri habari za punda akatufikiri sisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipofika kwenye inchi ya Zufu, Saulo alimwambia mutumishi wake: “Turudie kwetu. Kama si vile, baba yangu ataacha kufikiri juu ya punda na kuwa na wasiwasi juu yetu.”