1 Samuel 9:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mtumishi akamwambia, “Ngoja kidogo; katika mji huu kuna mtu wa Mungu ambaye anaheshimiwa sana; kila asemalo huwa kweli. Sasa tumwendee, labda anaweza kutuambia jinsi safari yetu itakavyokuwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mtumishi akajibu, “Tazama, katika mji huu yupo mtu wa Mungu, anayeheshimiwa sana na kila kitu asemacho kweli hutukia. Sasa na twende huko. Huenda atatuambia twende njia ipi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akamwambia, Tazama, katika mji huu mna mtu wa Mungu, naye ni mtu mwenye kuheshimiwa; yote asemayo hutukia kweli kweli; basi, twende huko; labda yeye aweza kutuambia habari ya safari yetu tunayoiendea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mtumishi akamwambia, “Ngoja kidogo; katika mji huu kuna mtu wa Mungu ambaye anaheshimiwa sana; kila asemalo huwa kweli. Sasa tumwendee, labda anaweza kutuambia jinsi safari yetu itakavyokuwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mtumishi akajibu, “Tazama, katika mji huu yupo mtu wa Mungu, anayeheshimiwa sana na kila kitu asemacho hutokea kweli. Sasa na twende huko. Huenda atatuambia twende njia ipi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mtumishi akajibu, “Tazama, katika mji huu yupo mtu wa Mungu, anayeheshimiwa sana na kila kitu asemacho hutokea kweli. Sasa na twende huko. Huenda atatuambia twende njia ipi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akamwambia, Tazama, katika mji huu mna mtu wa Mungu, naye ni mtu anaheshimiwa; yote asemayo hutukia hakika; basi, twende huko; labda yeye anaweza kutuambia kuhusu safari yetu tunayoiendea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mtumishi akamwambia, “Ngoja kidogo; katika mji huu kuna mtu wa Mungu ambaye anaheshimiwa sana; kila asemalo huwa kweli. Sasa tumwendee, labda anaweza kutuambia jinsi safari yetu itakavyokuwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akamwambia: Tazama! Humu mjini yumo mtu wa Mungu, naye ni mwenye macheo, kwani yote, anayoyasema, hutimia; sasa twende huko, labda atatuonyesha njia, tutakayoishika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akamwambia, Tazama, katika mji huu mna mtu wa Mungu, naye ni mtu mwenye kuheshimiwa; yote asemayo hutukia kweli kweli; basi, twende huko; labda yeye aweza kutuambia habari ya safari yetu tunayoiendea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mutumishi akamwambia: “Ngoja kidogo. Katika muji huu kuna mutu wa Mungu ambaye anaheshimiwa sana. Kila neno analosema linakuwa kweli. Sasa tumwendee. Labda anaweza kutuambia jinsi safari yetu itakavyokuwa.”