1 Thessalonians 1:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Paulo, Silwano na Timotheo, kwa jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambayo ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo. Tunawatakieni neema na amani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kundi la waumini la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu, Baba yetu, na ndani ya Bwana wetu Isa Al-Masihi. Neema iwe kwenu na amani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Paulo, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Salamu toka kwa Paulo, Sila, na Timotheo. Kwa kanisa lililoko Thesalonike lililo milki ya Mungu baba na Bwana Yesu Kristo. Neema na amani ziwe zenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi Paulo, Silwano na Timotheo tunawaandikia ninyi jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambao ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Paulo, Silwano na Timotheo, kwa jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambayo ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo. Tunawatakieni neema na amani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paulo, Silvano na Timotheo: Kwa kanisa la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu Baba yetu na ndani ya Bwana Yesu Kristo: Neema iwe kwenu na amani, itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paulo, Silvano na Timotheo: Kwa kundi la waumini la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu Baba yetu, na ndani ya Bwana Isa Al-Masihi: Neema iwe kwenu na amani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Paulo, Silwano na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Paulo, Silwano na Timotheo, kwa jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambayo ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo. Tunawatakieni neema na amani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sisi Paulo na Silwano na Timoteo tunawaandikia ninyi mlio wateule wa Tesalonike katika Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. Upole uwakalie na utengemano!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Paulo, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Barua hii inatoka kwangu mimi Paulo na kwa Silvano na Timoteo. Tunawaandikia ninyi kanisa la Tesalonika munaoungana na Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo. Tunawatakia neema na amani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
PAOLO, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathessaloniki, katika Mungu Baba, na Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.