1 Thessalonians 1:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
maana wakati tulipowahubirieni ile Habari Njema haikuwa kwa maneno tu, bali pia kwa nguvu na kwa Roho Mtakatifu, tukiwa na hakika kwamba ujumbe huo ulikuwa wa kweli. Mnajua jinsi tulivyoishi pamoja nanyi; tuliishi kwa manufaa yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho wa Mungu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda kati yenu kwa ajili yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tulipowaletea Habari Njema kwenu, tulikuja na yaliyo zaidi ya maneno. Tuliwaletea ile Habari Njema yenye uweza, pamoja na Roho Mtakatifu, na tulikuwa na uhakika kamili hiyo ilikuwa ni Kweli halisi. Pia mnafahamu tulivyo enenda tulipo kuwa pamoja nanyi. Tuliishi hivyo ili kuwasaidia ninyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
maana wakati tulipowahubirieni ile Habari Njema haikuwa kwa maneno tu, bali pia kwa nguvu na kwa Roho Mtakatifu, tukiwa na hakika kwamba ujumbe huo ulikuwa wa kweli. Mnajua jinsi tulivyoishi pamoja nanyi; tuliishi kwa manufaa yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
maana wakati tulipowahubirieni ile Habari Njema haikuwa kwa maneno tu, bali pia kwa nguvu na kwa Roho Mtakatifu, tukiwa na hakika kwamba ujumbe huo ulikuwa wa kweli. Mnajua jinsi tulivyoishi pamoja nanyi; tuliishi kwa manufaa yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho Mtakatifu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda katikati yenu kwa ajili yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho wa Mwenyezi Mungu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda katikati yenu kwa ajili yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ya kwamba Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
maana wakati tulipowahubirieni ile Habari Njema haikuwa kwa maneno tu, bali pia kwa nguvu na kwa Roho Mtakatifu, tukiwa na hakika kwamba ujumbe huo ulikuwa wa kweli. Mnajua jinsi tulivyoishi pamoja nanyi; tuliishi kwa manufaa yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Utume wetu mwema haukuwa kwenu katika maneno tu, ila ulitenda hata nguvu, ukawapo nayo Roho takatifu, mkapata pa kujishikizia sana; mwajua, tulivyokuwa kwenu kwa ajili yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana tulipohubiri Habari Njema kwenu, hatukuihubiri kwa maneno tu, lakini kwa uwezo na kwa musaada wa Roho Mutakatifu na kwa uhakika kabisa. Munajua namna gani tulivyoishi katikati yenu, kusudi tupate kuwafalia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthubutifu mwingi; kama mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.