1 Thessalonians 1:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, kutokana na bidii yenu ujumbe wa Bwana umesikika si huko Makedonia na Akaya tu, bali imani yenu kwa Mungu imeenea popote. Tena hatuhitaji kusema zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana kutoka kwenu neno la Bwana Isa limesikika, si katika Makedonia na Akaya tu, bali pia imani yenu katika Mungu imejulikana kila mahali, kiasi kwamba hatuna haja ya kusema chochote juu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mafundisho ya Bwana yameenea toka Makedonia mpaka Akaya na nje ya mipaka yake. Kwa kweli, imani yenu katika Mungu imejulikana kila mahali, hivyo hatuna haja ya kumwambia mtu yeyote kwa habari hii.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, kutokana na bidii yenu ujumbe wa Bwana umesikika si tu huko Makedonia na Akaya, bali imani yenu kwa Mungu imeenea popote. Tena hatuhitaji kusema zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, kutokana na bidii yenu ujumbe wa Bwana umesikika si huko Makedonia na Akaya tu, bali imani yenu kwa Mungu imeenea popote. Tena hatuhitaji kusema zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana kutoka kwenu Neno la Mungu limesikika, si katika Makedonia na Akaya tu, bali pia imani yenu katika Mungu imejulikana kila mahali kiasi kwamba hatuna haja ya kusema lo lote kwa habari yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana kutoka kwenu neno la Bwana Isa limesikika, si katika Makedonia na Akaya tu, bali pia imani yenu katika Mwenyezi Mungu imejulikana kila mahali kiasi kwamba hatuna haja ya kusema lolote kwa habari yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lolote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, kutokana na bidii yenu ujumbe wa Bwana umesikika si huko Makedonia na Akaya tu, bali imani yenu kwa Mungu imeenea popote. Tena hatuhitaji kusema zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani uvumi wa Neno la Bwana ulitoka kwenu, ukaenea Makedonia na Akea, lakini si huko tu, ila imejulikana waziwazi po pote, mnavyomtegemea Mungu. Kwa hiyo haitupasi sisi kuvisema mahali po pote,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana tokea kwenu neno la Bwana lilienea, si katika Makedonia na Akaya tu, lakini habari za imani kwa Mungu zilisambaa fasi zote, hata sisi hatukukuwa tena na lazima ya kusema neno juu ya ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana kutoka kwenu Neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu: bali na katika killa mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea, hatta hatuna haja sisi kunena lo lote.