1 Thessalonians 2:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, kwamba mwenendo wetu kati yenu nyinyi mnaoamini ulikuwa mzuri, mwadilifu na bila lawama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninyi wenyewe ni mashahidi na Mungu pia, jinsi tulivyokuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama miongoni mwenu ninyi mlioamini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tulipokuwa pamoja nanyi enyi mnaoamimi, tulikuwa safi, wa kweli, na wasio na kosa lolote kwa namna tulivyoishi maisha matakatifu. Mnafahamu, kama vile Mungu anavyotenda, kuwa jambo hili ni la kweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, jinsi mwenendo wetu kati yenu ninyi mnaoamini ulivyokuwa mzuri, mwadilifu na usio na lawama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, kwamba mwenendo wetu kati yenu nyinyi mnaoamini ulikuwa mzuri, mwadilifu na bila lawama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninyi wenyewe ni mashahidi na Mungu pia, jinsi tulivyokuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama miongoni mwenu ninyi mlioamini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninyi wenyewe ni mashahidi na Mungu pia, jinsi tulivyokuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama miongoni mwenu ninyi mlioamini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, kwamba mwenendo wetu kati yenu nyinyi mnaoamini ulikuwa mzuri, mwadilifu na bila lawama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi pamoja na Mungu m mashahidi, jinsi tulivyowaendea ninyi mmtegemeao, maana tulikuwa wenye kumcha Mungu na wenye wongofu, mtu asione la kutuonya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi ni washuhuda wetu, na Mungu vilevile anashuhudia kwamba tulipokaa kati yenu ninyi waamini, tuliishi katika utakatifu na haki, na bila kosa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ninyi mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;