1 Thessalonians 2:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, nyinyi mmepatwa na mambo yaleyale yaliyoyapata makanisa ya Mungu kule Yudea, mambo yaliyowapata watu walio wake Kristo Yesu. Nyinyi mlidhulumiwa na wananchi wenzenu kama vile wao walivyodhulumiwa na wenzao Wayahudi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana ninyi ndugu zetu, mlifanyika wafuasi wa makundi ya waumini wa Mungu walio ndani ya Al-Masihi Isa katika Yudea. Mlipata mateso yale yale kutoka kwa watu wenu wenyewe kama vile waumini hao walivyoteswa na Wayahudi,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kaka na dada zangu katika Bwana, mmeufuata mfano wa makanisa ya Mungu yaliyoko Uyahudi yaliyo mali ya Kristo Yesu. Nina maana ya kuwa ninyi mlitendewa vibaya na watu wa kwenu, namna ile ile walioamini wa Kiyahudi walivyotendewa vibaya na Wayahudi wenzao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, ninyi mmepatwa na mambo yaleyale yaliyoyapata makanisa ya Mungu kule Yudea, mambo yaliyowapata watu walio wake Kristo Yesu. Ninyi mlidhulumiwa na wananchi wenzenu kama vile wao walivyodhulumiwa na wenzao Wayahudi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, nyinyi mmepatwa na mambo yaleyale yaliyoyapata makanisa ya Mungu kule Yudea, mambo yaliyowapata watu walio wake Kristo Yesu. Nyinyi mlidhulumiwa na wananchi wenzenu kama vile wao walivyodhulumiwa na wenzao Wayahudi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ninyi ndugu zetu, mlifanyika wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyoko ndani ya Kristo Yesu katika Uyahudi. Mlipata mateso yale yale kutoka kwa watu wenu wenyewe kama vile makanisa hayo yalivyoteswa na Wayahudi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana ninyi ndugu zetu, mlifanyika wafuasi wa makundi ya waumini ya Mungu yaliyoko ndani ya Al-Masihi Isa katika Uyahudi. Mlipata mateso yale yale kutoka kwa watu wenu wenyewe kama vile waumini hao walivyoteswa na Wayahudi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yudea, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, nyinyi mmepatwa na mambo yaleyale yaliyoyapata makanisa ya Mungu kule Yudea, mambo yaliyowapata watu walio wake Kristo Yesu. Nyinyi mlidhulumiwa na wananchi wenzenu kama vile wao walivyodhulumiwa na wenzao Wayahudi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ninyi ndugu, mmepata kufanana na wateule wa Mungu walio wake Kristo Yesu katika nchi ya Yudea, kwani nanyi mmeteswa yaleyale na wenzenu wa kabila, kama nao wale walivyoteswa na Wayuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu, mambo yale yale yaliyotokea makanisa ya Mungu ya Yudea yanayoungana na Yesu Kristo, ndiyo yaliyowatokea ninyi vilevile. Kwa maana ninyi muliteswa na wanainchi wenzenu kama vile wao walivyoteswa na wanainchi wenzao Wayuda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana uinyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu, waliyopata na hao kwa Wayahudi;