1 Thessalonians 2:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni maadui za kila mtu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wale waliomuua Bwana Isa na manabii, nasi wakatufukuza pia. Watu hao walimchukiza Mungu na tena ni adui wa watu wote,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wayahudi wengine pia walimuua Bwana Yesu na manabii. Na walitulazimisha sisi kuondoka katika mji lenu. Hawampendezi Mungu, na wako kinyume na watu wengine wote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni adui za kila mtu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni maadui za kila mtu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wale waliomwua Bwana Yesu na manabii, nasi wakatufukuza pia. Watu hao walimchukiza Mungu na tena ni adui wa watu wote,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wale waliomuua Bwana Isa na manabii, nasi wakatufukuza pia. Watu hao walimchukiza Mungu na tena ni adui wa watu wote,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wowote;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni maadui za kila mtu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndio wao hao waliomwua naye Bwana Yesu, hata wafumbuaji, tena ndio waliotufukuza na sisi; hawampendezi Mungu kwa kupingana na watu wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ndio wale waliomwua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa sisi vilevile. Wao hawamupendezi Mungu, nao ni waadui za watu wote!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
waliomwua Bwana Yesu na manabii wao wenyewe na kutuudhi sisi, wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;