1 Thessalonians 2:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, kuachana kwetu nanyi kulikuwa kwa muda tu, tena kuachana huko kulikuwa kwa mwili tu na si kwa roho. Kitambo kifupi baadaye, tulishikwa na hamu kubwa ya kuwaoneni tena!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ndugu zetu, tulipotenganishwa nanyi kwa muda mfupi (ingawa kutengana huko kulikuwa kwa mwili tu, si kwa moyo), tulizidi kuwa na shauku kubwa kuwaona uso kwa uso.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sisi, ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa kitambo, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kaka na dada zangu, tulikuwa kama yatima, tulitengwa nanyi kwa muda. Lakini hata kama hatukuwa pamoja nanyi, mawazo yetu yalikuwa bado yangali nanyi. Tulitamani sana kuwaona, na tulijitahidi sana kulitimiza hilo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, kuachana kwetu nanyi kulikuwa kwa muda tu, tena kuachana huko kulikuwa kwa mwili tu na si kwa roho. Kitambo kifupi baadaye, tulishikwa na hamu kubwa ya kuwaoneni tena!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, kuachana kwetu nanyi kulikuwa kwa muda tu, tena kuachana huko kulikuwa kwa mwili tu na si kwa roho. Kitambo kifupi baadaye, tulishikwa na hamu kubwa ya kuwaoneni tena!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ndugu zetu, tulipotenganishwa nanyi kwa kitambo kidogo (ingawa kutengana huko kulikuwa kwa mwili tu, si kwa moyo), tulizidi kuwa na shauku kubwa kuwaona uso kwa uso.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ndugu zetu, tulipotenganishwa nanyi kwa kitambo kidogo (ingawa kutengana huko kulikuwa kwa mwili tu, si kwa moyo), tulizidi kuwa na shauku kubwa kuwaona uso kwa uso.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sisi, ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa muda, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, kuachana kwetu nanyi kulikuwa kwa muda tu, tena kuachana huko kulikuwa kwa mwili tu na si kwa roho. Kitambo kifupi baadaye, tulishikwa na hamu kubwa ya kuwaoneni tena!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sisi ndugu tumetengwa nanyi kitambo cha sasa, tusionane nanyi uso kwa uso, lakini mioyo haikutengwa; kwa hiyo tulijipingia sana kuonana nanyi uso kwa uso, kwani tuliwatunukia sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sisi, ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa kitambo, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu, sisi kwa ngambo yetu, tuliachana nanyi kwa muda kimwili, lakini si kiroho. Nyuma ya pale tulifanya bidii sana kusudi tuwafikie.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini sisi, ndugu, tukifarakana nanyi kwa kitambo, kwa nso si kwa moyo, tulitamani zaidi kuwaona nyuso zenu, kwa shauku nyingi.