1 Thessalonians 2:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, tutakaposimama mbele ya Bwana Yesu wakati atakapokuja, fahari ya ushindi wetu itakuwa nini? Itakuwa ni nyinyi wenyewe; nyinyi ndio tumaini letu na furaha yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana tumaini letu ni nini, au furaha yetu, au taji letu la kujisifia mbele za Bwana wetu Isa Al-Masihi wakati wa kuja kwake? Je, si ni ninyi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji ya kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninyi ni tumaini letu, furaha yetu, na taji yetu tutakayojivunia wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, tutakaposimama mbele ya Bwana Yesu wakati atakapokuja, fahari ya ushindi wetu itakuwa nini? Itakuwa ni ninyi wenyewe; ninyi ndio tumaini letu na furaha yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, tutakaposimama mbele ya Bwana Yesu wakati atakapokuja, fahari ya ushindi wetu itakuwa nini? Itakuwa ni nyinyi wenyewe; nyinyi ndio tumaini letu na furaha yetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana tumaini letu ni nini, au furaha yetu au taji yetu ya kujisifia mbele za Bwana Yesu Kristo wakati wa kuja kwake? Je, si ninyi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana tumaini letu ni nini, au furaha yetu au taji yetu ya kujisifia mbele za Bwana Isa Al-Masihi wakati wa kuja kwake? Je, si ni ninyi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji la kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, tutakaposimama mbele ya Bwana Yesu wakati atakapokuja, fahari ya ushindi wetu itakuwa nini? Itakuwa ni nyinyi wenyewe; nyinyi ndio tumaini letu na furaha yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kingojeo chetu au furaha yetu au kilemba, tujivuniacho mbele ya Bwana wetu Yesu Kristo, atakapokuja, ndio nini, msipokuwa ninyi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji ya kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi peke yenu tu ndio tumaini, furaha, na taji ya ushindi tutakavyojivunia wakati Bwana Yesu Kristo atakaporudia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana tumnini letu, au furaha yetu, an taji ya kujisifu ni nini? Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu Kristo wakati wa kuja kwake?