1 Thessalonians 2:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana kama mjuavyo, sisi hatukutumia maneno ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mnavyojua, hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli ili kuficha tamaa mbaya; Mungu ndiye shahidi yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnafahamu kuwa hatukujaribu kuwarubuni kwa kusema mambo mazuri juu yenu. Hatukuwa tunatafuta jinsi ya kuzichukua pesa zenu. Hatukutumia maneno ama matendo kuficha tamaa yetu. Mungu anajua ya kuwa huu ni ukweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi mnajua kwamba sisi hatukuja kwenu na maneno matamu ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana kama mjuavyo, sisi hatukutumia maneno ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mjuavyo na Mungu akiwa shahidi yetu hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli kwa ajili ya kuficha tamaa mbaya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mjuavyo, hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli ili kuficha tamaa mbaya: Mungu ndiye shahidi yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wowote, kama mjuavyo, wala maneno ya juu juu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana kama mjuavyo, sisi hatukutumia maneno ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hatukutumia maneno matamutamu ya kujipendezesha kwenu, kama mnavyojua, wala hatukujitendekeza kama wenye kuficha choyo; hapa Mungu ndiye anayetushuhudia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vile munavyojua, hata siku moja hatukutumia masemi ya kujipendekeza kwa watu wala hatukutamani kupata mali kwa uficho; Mungu ni mushuhuda wetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya kuficha tamaa; Muugu ni shahidi.