1 Thessalonians 2:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tuliwapenda nyinyi sana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tu Habari Njema ya Mungu, bali pia na maisha yetu. Ndivyo mlivyokuwa wapenzi wetu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tuliwapenda sana, kiasi kwamba tulifurahia kushirikiana nanyi, si Injili ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa sababu mlikuwa wa thamani mno kwetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ilikuwa ni upendo wetu mkuu sana kwenu uliotufanya tuwashirikishe Habari Njema za Mungu. Zaidi ya hayo yote tulifurahi kuwashirikisha ninyi nafsi zetu wenyewe. Hiyo inadhihirisha ni kwa kiwango gani tuliwapenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tuliwapenda ninyi sana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tu Habari Njema ya Mungu, bali pia na maisha yetu. Ndivyo mlivyokuwa wapenzi wetu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tuliwapenda nyinyi sana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tu Habari Njema ya Mungu, bali pia na maisha yetu. Ndivyo mlivyokuwa wapenzi wetu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tuliwapenda sana kiasi kwamba tulifurahia kushirikiana nanyi, si Injili ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa sababu mlikuwa wa thamani mno kwetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tuliwapenda sana kiasi kwamba tulifurahia kushirikiana nanyi, si Injili ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa sababu mlikuwa wa thamani mno kwetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo ndivyo nasi tukiwajali kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tuliwapenda nyinyi sana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tu Habari Njema ya Mungu, bali pia na maisha yetu. Ndivyo mlivyokuwa wapenzi wetu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vivyo hivyo na sisi tuliwatunukia ninyi, tukataka sana kuwagawia Utume mwema wa Mungu, hata mioyo yetu nayo, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sisi tunawapenda sana hata tumekuwa tayari, si kuwatolea Habari Njema ya Mungu tu, lakini kutoa maisha yetu kwa ajili yenu vilevile. Ni vile kwa sababu ninyi mumekuwa kweli wapendwa wetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Vivyo hivyo sisi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapeni, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.