1 Thessalonians 3:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndio maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na hivyo nilimtuma nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi aliwajaribuni na kazi yote tuliyofanya miongoni mwenu ikapotea bure!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu hii niliposhindwa kuvumilia zaidi, nilimtuma mtu ili nipate habari za imani yenu. Niliogopa kwamba kwa njia fulani yule mjaribu asiwe amewajaribu, nasi tukawa tumejitaabisha bure.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii ndiyo sababu nilimtuma Timotheo kwenu, ili nipate kujua juu ya uaminifu wenu. Nilimtuma kwenu nilipokuwa siwezi kuendelea kusubiri zaidi. Nilihofu kuwa Shetani angeweza kuwashinda kwa majaribu yake. Kisha kazi yetu iliyokuwa ngumu ingepotea bure.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndio maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na hivyo nilimtuma nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi aliwajaribuni na kazi yote tuliyofanya miongoni mwenu imepotea bure!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndio maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na hivyo nilimtuma nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi aliwajaribuni na kazi yote tuliyofanya miongoni mwenu ikapotea bure!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu hii nilipokuwa siwezi kuvumilia zaidi, nilimtuma mtu ili nipate habari za imani yenu. Niliogopa kwamba kwa njia fulani yule mjaribu asiwe amewajaribu, nasi tukawa tumejitaabisha bure.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu hii nilipokuwa siwezi kuvumilia zaidi, nilimtuma mtu ili nipate habari za imani yenu. Niliogopa kwamba kwa njia fulani yule mjaribu asiwe amewajaribu, nasi tukawa tumejitaabisha bure.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nilituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndio maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na hivyo nilimtuma nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi aliwajaribuni na kazi yote tuliyofanya miongoni mwenu ikapotea bure!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nami sikuweza kuvumilia tena, nikamtuma, nipate kutambua, kama mwamtegemea Mungu bado, au kama yule mwenye kujaribu amewajaribu, masumbuko yetu ya kwenu yakawa ya bure.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni kwa sababu hiyo, nilipoona kwamba siwezi kuendelea kungojea, nilimutuma Timoteo kusudi nipate kujua habari ya imani yenu. Niliogopa kwamba labda yule mushawishi Shetani amejaribu kuwaangusha ninyi na kwamba kazi yote tuliyofanya kwenu imepotea bure.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalimtuma mtu illi niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, wala taabu yetu isiwe haina faida.