1 Thessalonians 3:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha kuhusu imani na upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na kwamba mna hamu ya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Timotheo amerejea kwetu hivi sasa kutoka kwenu, na ameleta habari njema kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuambia kwamba siku zote mnatukumbuka kwa wema, na kwamba mna shauku ya kutuona kama vile sisi tulivyo na shauku ya kuwaona ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Timotheo alipotujia hivi sasa kutoka kwenu, alituletea habari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote; mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi kuwaona ninyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Bali sasa Timotheo amerudi kutoka kwenu na kutueleza juu ya uaminifu wenu na upendo wenu. Ametueleza kuwa mmeendelea kuwa na kumbukumbu njema juu yetu kama mfano kwenu. Na amesema kuwa mnatamani sana kutuona tena. Hivyo ndivyo ilivyo kwetu pia tunatamani sana kuwaona ninyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha kuhusu imani na upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na kwamba mna hamu ya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha kuhusu imani na upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na kwamba mna hamu ya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa Timotheo ndiyo tu amerejea kwetu kutoka kwenu na ameleta habari njema kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuambia kwamba siku zote mnatukumbuka kwa wema na kwamba mna shauku ya kutuona kama vile sisi tulivyo na shauku ya kuwaona ninyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa Timotheo ndiyo tu amerejea kwetu kutoka kwenu na ameleta habari njema kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuambia kwamba siku zote mnatukumbuka kwa wema na kwamba mna shauku ya kutuona kama vile sisi tulivyo na shauku ya kuwaona ninyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Timotheo alipotujia hivi sasa kutoka kwenu, alituletea Habari Njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote; mkitamani kutuona kama vile nasi tunavyotamani kuwaona ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha kuhusu imani na upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na kwamba mna hamu ya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sasa Timoteo amefika kwetu kutoka kwenu, akatusimulia vema mambo mema, mnavyomtegemea Mungu, mnavyopendana, mnavyotukumbuka vema siku zote mkitunukia kutuona sisi, kama sisi tunavyotunukia kuwaona ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Timotheo alipotujia hivi sasa kutoka kwenu, alituletea habari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote; mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi kuwaona ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa Timoteo amefika kwetu, akirudia toka kule kwenu. Ametuletea habari nzuri juu ya imani yenu na upendo wenu. Ametuelezea kwamba munatukumbuka vizuri siku zote, na kwamba muko na hamu sana ya kutuona, kama vile sisi nasi tunavyokuwa na hamu ya kuwaona.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini Timotheo alipotujia siku hizi kutoka kwenu, akatuletea khabari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote: mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi ninyi;