1 Thessalonians 3:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, habari za imani yenu zimetutia moyo katika taabu na mateso yetu yote,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, ndugu zetu, katika dhiki na mateso yetu yote tumefarijika kwa sababu ya imani yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo, ndugu, tulifarijiwa kwa habari zenu, katika msiba na dhiki yetu yote, kwa imani yenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hiyo, ndugu zangu, tunatiwa moyo sana kwa ajili ya uaminifu wenu. Tunapata mateso na masumbufu mengi, lakini bado tunatiwa moyo nanyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, habari za imani yenu zimetutia moyo katika taabu na mateso yetu yote,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, habari za imani yenu zimetutia moyo katika taabu na mateso yetu yote,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, ndugu zetu, katika dhiki na mateso yetu yote tumefarijika kwa sababu ya imani yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, ndugu zetu, katika dhiki na mateso yetu yote tumefarijika kwa sababu ya imani yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo, ndugu, katika dhiki na mateso yetu yote, katika habari zenu, tumefarijiwa kwa imani yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, habari za imani yenu zimetutia moyo katika taabu na mateso yetu yote,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hayo, ndugu, tumetulizwa mioyo kwa ajili yenu katika mahangaiko na maumivu yetu yote, tuliposikia, mnavyomtegemea Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo, ndugu, tulifarijiwa kwa habari zenu, katika msiba na dhiki yetu yote, kwa imani yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo wandugu, katika taabu na mateso tunayopata, tumefarijiwa nanyi kwa kusikia habari za imani yenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa sababu hiyo tulifarijiwa, ndugu, kwa khabari zenu, katika shidda na mateso yetu yote, kwa imani yenu.