1 Thessalonians 4:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenu wote kila mahali katika Makedonia. Basi, ndugu, tunawaombeni mfanye hata zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi kwa kweli mnawapenda ndugu wote katika Makedonia nzima. Lakini ndugu, tunawasihi mzidi sana kuwapenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ukweli ni kuwa, mnawapenda wanaoamini wote walioko Makedonia. Tunawatia moyo sasa, kuuonyesha upendo wenu zaidi na zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenu wote kila mahali katika Makedonia. Basi, ndugu tunawaombeni mfanye hata zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenu wote kila mahali katika Makedonia. Basi, ndugu, tunawaombeni mfanye hata zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi kwa kweli mnawapenda ndugu wote katika Makedonia nzima. Lakini ndugu, tunawasihi mzidi sana kuwapenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi kwa kweli mnawapenda ndugu wote katika Makedonia nzima. Lakini ndugu, tunawasihi mzidi sana kuwapenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini tunawasihi, ndugu, mzidi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenu wote kila mahali katika Makedonia. Basi, ndugu, tunawaombeni mfanye hata zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi mnawafanyia hivi ndugu wote katika nchi yote ya Makedonia. Lakini twawaonya ninyi, ndugu, lifulizieni jambo hili!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni vile mulivyojionyesha mbele ya wandugu wote wa kanisa la Makedonia. Na sasa tunawasihi ninyi wandugu, muendelee mbele vizuri zaidi katika jambo lile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia wote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana;