1 Thessalonians 4:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa namna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwa wale wasio Wakristo, na hamtakuwa na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu yeyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mkifanya mambo haya, ndipo wale wasioamini wataheshimu namna mnavyoishi. Na hamtawategemea wengine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa namna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwa wale wasio Wakristo, na hamtakuwa na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa namna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwa wale wasio Wakristo, na hamtakuwa na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu ye yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu yeyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili mwende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu chochote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa namna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwa wale wasio Wakristo, na hamtakuwa na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti mfanye mwenendo uwafaliao wale watu wa nje, kwao msitake mtu wo wote wa kuwasaidia.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi mutakuwa na mwenendo wa heshima mbele ya watu wasiokuwa wa Kristo, wala hamutahitaji kusaidiwa na mutu yeyote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illi mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na baja ya cho chote.