1 Thessalonians 4:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tunaamini kwamba Isa alikufa na kufufuka. Na kwa hivyo, tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja naye wale waliolala katika Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunaamini kuwa Yesu alikufa, ila tunaamini pia kuwa alifufuka. Hivyo tunaamini kuwa Mungu atawaleta katika uzima kupitia Yesu kila aliyekufa na kukusanywa pamoja naye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, hata hivyo, Mungu kwa njia ya Yesu atawafufua pamoja naye wale waliolala mauti katika yeye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa tunaamini kwamba Isa alikufa na kufufuka, na kwa hivyo, Mwenyezi Mungu kwa njia ya Isa atawafufua pamoja naye wale waliolala mautini ndani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, ikiwa tunaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani tukiyategemea, ya kuwa Yesu alikufa, kisha akafufuka tena, vivyo hivyo Mungu nao waliolala katika Yesu atawapeleka, wawe pamoja naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tunaamini kwamba Yesu alikufa na alifufuliwa, na kwa hiyo tunaamini vilevile kwamba Mungu atawafufua pamoja na Yesu wale waliokufa wakimwamini Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu Mungu atawaleta pamoja nae.