1 Thessalonians 4:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana, kwamba sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulingana na neno la Bwana Isa mwenyewe, tunawaambia kwamba sisi ambao bado tuko hai, tuliobaki hadi kuja kwake Bwana Isa, hakika hatutawatangulia waliolala katika mauti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunalowaambia sasa ni ujumbe wake Bwana. Sisi ambao bado tu hai Bwana ajapo tena tutaungana nae, lakini hatutawatangulia wale waliokwisha kufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana; sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki, wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana, kwamba sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kulingana na neno la Bwana mwenyewe tunawaambia kwamba, sisi ambao bado tuko hai, tutakaobaki hadi kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wale waliolala mauti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kulingana na neno la Bwana Isa mwenyewe, tunawaambia kwamba sisi ambao bado tuko hai, tuliobaki hadi kuja kwake Bwana Isa, hakika hatutawatangulia waliolala mauti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa tunawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana, kwamba sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani neno hili, tunalowaambia, ni neno lake Bwana kwamba: Sisi tunaoishi, tuliosazwa, mpaka Bwana atakapokuja, hatutawatangulia wale waliolala.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana, kufuatana na mafundisho ya Bwana, tunawaambia hivi: sisi tutakaokutiwa wazima wakati Bwana atakaporudia, hatutawatangulia wale waliokufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hayi, tutakaosalia hatta wakati wa kuja kwake Bwana, hatutawatangulia wao waliokwisha kulala.