1 Thessalonians 4:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Bwana Isa mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Al-Masihi watafufuka kwanza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Bwana mwenyewe atakuja kutoka mbinguni pamoja na sauti kuu yenye agizo, na sauti kubwa kutoka kwa malaika mkuu, na ishara ya Mungu ya mlio wa tarumbeta. Na watu waliokufa walio wake Kristo watafufuliwa kwanza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu pamoja na sauti ya malaika mkuu na sauti ya tarumbeta ya Mungu, nao wale waliolala mauti wakiwa wanamwamini Kristo watafufuka kwanza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Bwana Isa mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Al-Masihi watafufuka kwanza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni papo hapo, wito utakapovumika, nayo sauti ya malaika mkuu itasikilika, hata baragumu la Mungu litalia. Ndipo, waliokufa katika Kristo watakapofufuka kwanza;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu amri itakapotoka na sauti ya malaika mukubwa itakaposikilika, na baragumu ya Mungu itakapolia, Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni. Halafu wale waliokufa wakimwamini Kristo watafufuliwa kwanza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwasababu Bwana mwenyewe atasbuka kutoka mbinguni na sauti kuu na sauti ya malaika mkuu, na panda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo, watafufuliwa kwanza;