1 Thessalonians 4:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo basi, anayedharau mafundisho hayo hamdharau mtu, bali anamdharau Mungu mwenyewe anayewapeni Roho wake Mtakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, mtu yeyote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu, bali anamkataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo kila anayekataa kuyatii mafundisho haya anakataa kumtii Mungu, siyo wanadamu. Na Mungu ndiye anayewapa ninyi Roho Mtakatifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo basi, anayedharau mafundisho hayo hamdharau mtu, bali amdharau Mungu mwenyewe anayewapeni Roho wake Mtakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo basi, anayedharau mafundisho hayo hamdharau mtu, bali anamdharau Mungu mwenyewe anayewapeni Roho wake Mtakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, mtu ye yote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu, bali anamkataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, mtu yeyote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu, bali anamkataa Mwenyezi Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo basi, anayedharau mafundisho hayo hamdharau mtu, bali anamdharau Mungu mwenyewe anayewapeni Roho wake Mtakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, kwa hiyo mtu akiyatangua haya, hatangui ya mtu, ila yake Mungu aliyewapa ninyi Roho wake Mtakatifu, awakalie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kwa hiyo, yeye anayekataa mafundisho haya hamukatai mutu, lakini anamukataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mutakatifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi yeye anaekataa, hakatai mwana Adamu bali Mungu, anaewapeni Roho yake Mtakatifu.