1 Thessalonians 5:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Asiwepo anae jaribu kulipiza baya kwa baya. Lakini kila mara mfanye lililo jema kwa kila mmoja wenu na kwa watu wote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Angalieni kuwa mtu asilipe ovu kwa ovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwangalie, mtu asimlipe mwenziwe uovu kwa uovu! Ila siku zote myafuate yaliyo mema, myapatiane ninyi kwa ninyi, hata wengine wote!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muangalie vema, hata mumoja wenu asimurudishie mwenzake ubaya kwa ubaya, lakini mutafutiane wema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Angalieni mtu awae yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.