1 Thessalonians 5:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kuwa na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndio mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Al-Masihi Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Shukuruni kwa kila jambo. Hivi ndivyo Mungu anavyotutaka tuishi katika Kristo Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na muwe na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kuwa na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa ajili yenu katika Al-Masihi Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na kuwa na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mambo yote toeni shukrani! Kwani haya ndiyo, Mungu ayatakayo, myafanye, kwa kuwa wake Kristo Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumushukuru Mungu katika mambo yote. Kwa maana hayo ndiyo mambo Mungu anayotaka mufanye katika kuungana kwenu na Yesu Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
shukuruni kwa killa jambo; maana haya ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.