1 Thessalonians 5:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Mwenyezi Mungu itakuja kama mwizi anavyokuja usiku.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninyi mnafahamu vizuri kuwa siku ambayo Bwana atakuja itakuwa ya kushitukiza, kama mwizi anavyokuja usiku.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana ninyi wenyewe mwajua kwamba Siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwivi ajapo usiku.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana Mwenyezi itakuja kama mwizi ajapo usiku.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ninyi wenyewe mnajua hakika ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wenyewe mwajua sana: siku ya Bwana itafika, kama mwizi anavyokuja usiku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana munajua ninyi wenyewe kwamba siku Bwana atakaporudia, itatimia kwa saa musiyozania kama vile mwizi anavyokuja usiku.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku.