1 Thessalonians 5:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu mwenyewe anayetupatia amani awatakase nyinyi kabisa kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu — roho, mioyo na miili yenu — mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Isa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunaomba kwamba Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, atawafanya muwe watakatifu mkiwa wake. Tunaomba kwamba katika roho yote, nafsi yote, na mwili mzima mtahifadhiwa salama pasipo lawama Bwana wetu Yesu Kristo atakapokuja.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu anayetupatia amani awafanye ninyi watakatifu kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu—roho, mioyo na miili yenu—mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu mwenyewe anayetupatia amani awatakase nyinyi kabisa kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu — roho, mioyo na miili yenu — mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwenyezi Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Isa Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu mwenyewe anayetupatia amani awatakase nyinyi kabisa kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu – roho, mioyo na miili yenu – mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yeye Mungu aliye mwenye utengemano awatakase ninyi nyote miili na mioyo, kwamba roho zenu zote nzima pamoja na mioyo na miili zilindwe, zikae pasipo doadoa lo lote, mpaka Bwana wetu Yesu Kristo atakaporudi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa, alinde uzima wenu wote ndiyo roho, moyo na mwili wenu, kusudi visikutiwe na kosa wakati Bwana wetu Yesu Kristo atakaporudia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.