1 Thessalonians 5:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”, ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile uchungu unavyomjia mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu watasema, “tuna amani na tuko salama.” Wakati huo ndipo uharibifu utakapowajia haraka, kama maumivu anayoyapata mwanamke anapojifungua. Na watu hao hawataweza kukwepa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama” ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”, ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba wala hawatatoroka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”, ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakaposema: Pametengemana, pametulia, ndipo, watakapogunduliwa na mwangamizo, kama uchungu wa kuzaa unavyompata mwenye mimba; kwa hiyo hawataweza kukimbia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu watakapokuwa wakisema: “Kuna amani na usalama”, ndio wakati uharibifu utakapowapata kwa rafla kama vile maumivu ya kuzaa yanavyomupata mwanamuke mwenye mimba, wala hawataweza kuponyoka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo niwenye mimba; nao hawataokolewa.