1 Timothy 1:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wafiraji, wezi wa watu, waongo na wanaoapa uongo au wanaofanya chochote ambacho ni kinyume cha mafundisho sahihi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa wazinzi na wahanithi, kwa wale wauzao watu, na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa chochote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ipo kwa ajili ya watu wanaotenda dhambi ya uasherati, kwa wanaume wanaolala na wanaume wenzao au wavulana, kwa wote wanaoteka watu na kuwauza kama watumwa, kwa wote wanaodanganya au wale wasiosema ukweli wakiwa katika kiapo, na kwa ajili ya wale walio kinyume na mafundisho ya kweli ya Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wafiraji, wanaowaiba watu, waongo, na wanaoapa uongo au wanaofanya chochote ambacho ni kinyume cha mafundisho ya kweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wafiraji, wezi wa watu, waongo na wanaoapa uongo au wanaofanya chochote ambacho ni kinyume cha mafundisho sahihi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa wazinzi na wahanithi, wauza watu na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa cho chote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa wazinzi na wahanithi, kwa wale wauzao watu, na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa chochote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na linginelo lolote lisilopatana na mafundisho ya kweli;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wafiraji, wezi wa watu, waongo na wanaoapa uongo au wanaofanya chochote ambacho ni kinyume cha mafundisho sahihi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nao wagoni nao walalanao nao wauzao watu nao waongo nao waapao viapo vya uwongo, na kama wako wengine wafanyao neno jingine lisilopatana na ufundisho uwapao watu uzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wanaume wanaozini wao kwa wao, wenye kuuzisha watu, wasema uongo, wale wanaofanya viapo vya uongo na kwa ajili ya wote wanaofanya matendo yanayokuwa umbalimbali na mafundisho ya kweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na wazinzi, na wafiraji, na waibao watu, na wawongo, mi waapao uwongo, na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;