1 Timothy 1:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ingawa pale awali mimi nilimtukana na kumtesa na kumdhulumu. Lakini Mungu alinionea huruma, kwa sababu sikuwa na imani bado, na hivyo sikujua nilichokuwa ninafanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa wakati fulani nilikuwa mwenye kukufuru, mtesaji na mwenye jeuri, lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda hivyo kwa kutojua na kutoamini kwangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hapo zamani nilimtukana Kristo. Nikiwa mtu mwenye majivuno na mkorofi, niliwatesa watu wake. Lakini Mungu alinihurumia kwa sababu sikujua nilichokuwa nafanya. Nilifanya hayo kabla sijaamini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
ingawa pale awali mimi nilimtukana na kumtesa na kumdhulumu. Lakini Mungu alinionea huruma, kwa sababu sikuwa na imani bado, na hivyo sikujua nilichokuwa ninafanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ingawa pale awali mimi nilimtukana na kumtesa na kumdhulumu. Lakini Mungu alinionea huruma, kwa sababu sikuwa na imani bado, na hivyo sikujua nilichokuwa ninafanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa wakati fulani nilikuwa mwenye kukufuru, mtesaji na mwenye jeuri. Lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda hivyo kwa kutokujua na kutokuamini kwangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa wakati fulani nilikuwa mwenye kukufuru, mtesaji na mwenye jeuri, lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda hivyo kwa kutojua na kutoamini kwangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ingawa hapo awali nilikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye ujeuri, lakini nilipata rehema kwa kuwa nilifanya hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ingawa pale awali mimi nilimtukana na kumtesa na kumdhulumu. Lakini Mungu alinionea huruma, kwa sababu sikuwa na imani bado, na hivyo sikujua nilichokuwa ninafanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
niliyekuwa kale mwenye kuwatukana na kuwafukuza na kuwakorofisha walio wake. Lakini nilihurumiwa, kwani naliyafanya pasipo kujua maana, kwani nilikuwa sijamtegemea Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa zamani nilikuwa mwenye kumutukana, mwenye kumutesa na kumutendea kwa ukali, lakini amenihurumia, kwa sababu yote niliyofanya, niliyafanya kwa upumbafu kwa maana sikukuwa bado na imani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mimi niliyekuwa kwanza mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri: lakini nalirehemiwa kwa kuwa nalitenda hivyo kwa njinga, na kwa kutokuwa na imani;