1 Timothy 1:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwanangu Timotheo, nakukabidhi amri hii kufuatana na maneno ya unabii yaliyosemwa zamani juu yako. Yatumie maneno hayo yawe silaha yako katika kupigana vita vizuri,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwanangu Timotheo, ninakupa agizo hili, kwa kadiri ya maneno ya unabii yaliyosemwa kukuhusu, ili kwa kuyafuata upate kupigana vita vizuri,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo uvipige vile vita vizuri;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Timotheo wewe ni mwanangu mwenyewe kwa sababu ya ushirika wetu wa imani ya kweli. Ninayokuambia kuyatenda yanakubaliana na unabii ambao ulisemwa juu yako hapo zamani. Nataka uukumbuke unabii huo na kupigana vita vizuri vya imani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwanangu Timotheo, nakukabidhi amri hii kufuatana na maneno ya unabii yaliyosemwa zamani juu yako. Yatumie maneno hayo yawe silaha yako katika kupigana vita vizuri,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwanangu Timotheo, nakukabidhi amri hii kufuatana na maneno ya unabii yaliyosemwa zamani juu yako. Yatumie maneno hayo yawe silaha yako katika kupigana vita vizuri,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwanangu Timotheo, ninakupa agizo hili, kwa kadiri ya maneno ya unabii yaliyosemwa kukuhusu, ili kwa kuyafuata upate kupigana vile vita vizuri,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwanangu Timotheo, ninakupa agizo hili, kwa kadiri ya maneno ya unabii yaliyosemwa kukuhusu, ili kwa kuyafuata upate kupigana vita vizuri,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyonenwa awali juu yako, ili katika hayo uweze kupigana vile vita vizuri;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwanangu Timotheo, nakukabidhi amri hii kufuatana na maneno ya unabii yaliyosemwa zamani juu yako. Yatumie maneno hayo yawe silaha yako katika kupigana vita vizuri,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwanangu Timoteo, kwa ajili ya maneno ya ufumbuaji, uliyosemewa kale, nakupa agizo hili, uyashindanie mashindano mazuri
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo uvipige vile vita vizuri;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Timoteo mwana wangu, ninakupa agizo hili kufuatana na maneno ya unabii yaliyosemwa zamani juu yako. Maneno hayo ndiyo yatakayokuwezesha kupiga vita nzuri,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Agizo hilo nakupa iwe akiba, mwanangu Timotheo, kwa ajili ya maneno ya unabii yalivotangulia juu yako, illi katika hayo ufanye vile vita vizuri;