1 Timothy 1:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na ushike imani yako na dhamiri njema. Watu wengine hawakusikiliza dhamiri zao na hivyo wakaiharibu imani yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ukiishikilia imani na dhamiri safi, ambazo wengine wamevikataa, na hivyo wakaangamia kwa habari ya imani yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Endelea kumwamini Mungu na kutenda yale unayojua kuwa ni sahihi. Watu wengine hawajatenda haya, na imani yao sasa imeharibiwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na ushike imani yako na dhamiri njema. Watu wengine hawakusikiliza dhamiri zao na hivyo wakaiharibu imani yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na ushike imani yako na dhamiri njema. Watu wengine hawakusikiliza dhamiri zao na hivyo wakaiharibu imani yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ukiishikilia imani na dhamiri njema ambayo wengine wamevikataa na hivyo, wakaangamia kwa habari ya imani yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ukiishikilia imani na dhamiri njema, ambazo wengine wamevikataa, na hivyo wakaangamia kwa habari ya imani yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia katika Imani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na ushike imani yako na dhamiri njema. Watu wengine hawakusikiliza dhamiri zao na hivyo wakaiharibu imani yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ukiwa mwenye kumtegemea Mungu na wenye moyo ujuayo yaliyo mema tu. Wengine waliutupa moyo ulio hivyo, kwa hiyo nazo nguvu zao za kumtegemea Mungu zikatota;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ukichunga imani yako na kuwa na zamiri safi. Watu wamoja wamekataa kuwa na zamiri hata wamepoteza imani yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nwe mwenye imani na dhamiri njema; wengine wamezisukumia mbali hizo, wakavunja chombo cha imani.